Home Soka Waarabu Watua Kuivaa Yanga Sc

Waarabu Watua Kuivaa Yanga Sc

by Sports Leo
0 comments

Kikosi Cha Klabu ya Al Hilal Omdurman ya Sudan tayari kimewasili Tanzania alfajiri ya leo Novemba 20,2024 kwa ajili ya mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya Yanga SC utakaochezwa Novemba 26,2024 katika uwanja wa Benjamin mkapa.

Msafara wa watu zaidi ya Arobaini umetua mapema asubuhi ya Novemba 20 2024 katika uwanja wa ndege wa J.K Nyerere na jioni yake kufanya mazoezi katika uwanja wa J.K Park uliopo eneo la kidongo chekundu Kariakoo.

Mastaa wa kikosi hicho wakiwa na Kocha mzoefu Florent Ibenge wanatarajiwa kuwapa kazi nzito mastaa wa Yanga sc ambao wamejifungia kambini Avic Town wakinasa mbinu za kocha mpya Sead Ramovic ambazo watazitumia jioni ya Novemba 26 saa kumi jioni katika uwanja maarufu kwa sasa barani Afrika wa Benjamin Mkapa.

banner

Yanga sc wanapaswa kuwachunga Mohammed Abdulrahman na kiungo Serge Pokue ambao wamekua na viwango bora kabisa katika kikosi hicho.

Ikumbukwe Al Hilal Fc iliwahi kuwatoa Yanga sc katika hatua ya mtoano mwaka 2021 chini ya kocha Nasredine Nabi wakiwafunga ugenini bao 1-0 huku wakitoa sare nyumbani ya 1-1.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited