Kikosi cha Yanga Sc kinachonolewa na kocha mkuu, Zlatko Krmpotic kinatarajia kuanza safari yake leo kueleleka Morogoro kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa uwanja wa Jamhuri, Septemba 27, Jumapili.
Yanga sc inawafuata Mtibwa ikiwa imetoka kushinda bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar hivyo mchezo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kusaka pointi tatu.
Huku pia Mtibwa Sugar ikiwakaribisha Yanga kwa mara ya kwanza ndani ya msimu wa 2020/21 ikiwa imetoka kushinda bao 1-0 mbele ya Ihefu mchezo uliochezwa uwanja wa Sokoine.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.