Home Soka Yanga Sc Yamtambulisha Mwenda

Yanga Sc Yamtambulisha Mwenda

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imemtambulisha beki Israel Mwenda iliyemsajili kwa mkopo kutoka klabu ya Singida Black Stars kwa mkopo wa miezi sita mpaka mwisho wa msimu huu.

Punde tu baada ya kumtambulisha staa huyo moja kwa moja alijiunga na kambi ya timu hiyo kwa ajili ya mazoezi yanayofanyika katika uwanja wa Kmc Complex Jijini Dar es Salaam.

Katika mazoezi hayo Mwenda alionekana kuwa na furaha huku tayari akiwa amezoeana na baadhi ya wachezaji wenzake kama Nickson Kibabage na Cletous Chama waliyecheza nae pamoja Simba sc.

Mwenda anakwenda kuongeza nguvu hasa katika upande wa kulia na kushoto mwa safu ya ulinzi ya klabu hiyo sehemu ambapo kuna majeraha ya mara kwa mara ya Chadrack Boka na Yao Kouasi Attouhoula hali ambayo huwaacha Kibwana Shomari na Nickson Kibabage bila ushindani wowote.

banner

Kupeana wachezaji baina ya Yanga sc na Singida Black Stars imekua kawaida ambapo na sasa yapo mazungumzo ya usajili wa Kelvin Nashon kuja Yanga sc kwa mkopo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited