Home Makala Yanga Sc Yapaa Kwenda Afrika Kusini

Yanga Sc Yapaa Kwenda Afrika Kusini

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Yanga sc imeondoka nchini Tanzania mchana wa leo kuelekea nchini Afrika ya kusini kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya mwanzo wa msimu pamoja na kucheza michezo kadhaa ya kirafiki ikiwa nchini humo.

Mastaa wa klabu hiyo waliwasili uwanjani hapo mchana wa leo na hivi sasa tayari wapo anngani kuelekea nchini humo ambapo watashiriki michuano maalumu ya Toyota Cup huku pia wakipata wasaa wa kucheza na timu ya Augusburg inayoshiriki ligi kuu ya Bundesliga nchini Ujerumani.

banner

Mastaa wapya wakiwemo Prince Dube,Jean Baleke,Cletous Chama,Duke Abuya ni miongoni mwa wachezaji waliosafiri na kikosi hicho na sasa tayari wanaelekea eneo la Mpumalanga kwa ajili ya kushiriki michuano maalumu ya Mpumalanga Cup.

Kikosi hicho pia kitakua na michezo mbalimbali ya kirafiki kupitia michuano hiyo miwili na kinatarajiwa kuwasili nchini mwanzoni mwa mwezi wa nane kwa ajili ya Tamasha la Yanga day linalotarajiwa kufanyika Augusti 4 katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited