Home Masumbwi Bondia Mwingine Afariki Baada ya Pambano

Bondia Mwingine Afariki Baada ya Pambano

by Sports Leo
0 comments

Bondia kutoka nchini Ajentina Hugo Santillan mwenye umri wa miaka 23 amefariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kupambana na Eduardo Abreau taarifa iliyothibitishwa na shirikisho la ngumi duniani.

Bondia huyo amefariki siku mbili baada ya bondia mwenye asili ya Urusi Maxim Dadashev kufariki kwa majeraha aliyopata baada ya kupambana na  Subriel Matias katika pamboni lililiofanyika katika ukumbi wa Mgm nchini Marekani.

Bondia huyo  alizirai katika ukumbi siku ya Jumamosi baada ya pigano lake la ukanda wa WBC dhidi ya Eduardo Javier Abreu nchini Argentina kuisha kwa sare.Alipelekwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji lakini akafariki siku ya Alhamisi.

banner

Akiwa ameanguka chini wakati majaji wakitangaza matokeo.

Santillan ni bondia wa pili kufariki kutokana na majeraha aliyopata katika ulingo wa ndondi wiki hii baada ya kifo cha Dadashev kuthibitishwa siku ya Jumanne.

Shirikisho la ndondi duniani lilisema”Tumepokea taarifa za kuhudhunisha za bondia Hugo Santillan kutoka nchini Ajentina,tunawatakia pole na huruma familia yake na rafiki zake katika kipindi hiki kigumu”.

Repoti kutoka jijini Buenos Aroes mji mkuu wa nchi hiyo zinadai Hugo alianza kutokwa na damu puani katika raundi ya nne katika pambano la raundi kumi na ingawa alinyosha mkono lakini alianguka wakati majaji wakisoma matokeo hayo ya sare.

“Toka aletwe hospitali figo imefeli na amekua katika hali ya kutojitambua muda wote”Alisema Dokta Glaciera Olloco kutoka hospitali ya  Agudos San Felipe.

Santillan,Bondia wa uzito wa kati ni mtoto wa bondia wa zamani Alfredo Santillan na amepambana katika mapambano 27 toka mwaka 2015 akishinda mapambano nane kwa Ko’s.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited