Home Masumbwi Bondia Mwingine Afariki Ulingoni

Bondia Mwingine Afariki Ulingoni

by Sports Leo
0 comments

Bondia wa Marekani Patrick Day 27,ambaye alikuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi tangu siku ya Jumamosi usiku baada ya kujeruhiwa vibaya katika pambano la ndondi ya kulipwa amefariki.

Bondia huyo alipigwa na mpinzani wake Charles Conwell akapoteza fahamu ulingoni katika roundi ya 10 katika pambano la Superwelter weight lililofanyika chicago nchini marekani ambapo alianguka na kupoteza fahamu mpaka alipofariki kutokana na majeraha katika ubongo ambapo alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya westernnorth memorial Hospital nchini humo lakini alifariki dunia.

Mwaka 2019 umekua mchungu kwa tasnia ya ngumi ambapo mpaka sasa mabondia watatu wamefariki ulingoni akiwemo day wengine bondia muajentina Hugo Santillan aliyefariki mwezi julai huku mburgalia Boris Stanchov akifariki mwezi wa tisa baada ya kupigwa ulingoni.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited