Kiungo Rasta mzimbabwe Thabani Kamusoko anasubiria kumalizika kwa Michuano ya Afrika (Afcon) ili kujua hatima yake ya klabu atakayoichezea msimu ujao.
Kiungo huyo mwenye amesema tayari ana ofa tatu mezani licha ya klabu yake ya Yanga kutomtafuta kwa ajili ya kuongeza mkataba mpya baada ya ule wa awali wa miaka miwili kufikia tamati.
Kamusoko ambaye yupo na timu ya taifa ya Zimbabwe nchini Misri amesema kuwa ameipa nafasi kwanza michuano hiyo kisha ikimalizika ndio ataangalia ofa ipi ni nzuri japo ofa hizo mbili kati ya tatu zinafanana.
“Bado sijasaini popote japo kuna ofa tatu mbili ni nzuri na zinalingana lakini nitaamua pa kwenda baada ya fainali hizi kukamilika”alisema kamusoko.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kamusoko alijiunga na Yanga iliyokua chini kocha Hans van Pluijm mwaka 2015 na ameichezea timu hiyo kwa miaka minne na kufanikiwa kuipa taji la ligi kuu mara tatu mfululizo.