Home Soka Chama Aomba Radhi

Chama Aomba Radhi

by Sports Leo
0 comments

Kiungo wa Simba Clatous Chama amemuomba radhi kiungo fundi Feisal Salum ‘Fei Toto’ kufuatia tukio la kumkanyaga makusudi kwenye mchezo baina ya timu hizo uliopigwa uwanja wa Taifa Jumapili ya March 08

Chama amethibitisha kuwa aliongea na Feisal na akamuomba radhi mapema jana lakini pia akatumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kuomba radhi mbele ya mashabiki ambao wengi wamekerwa na tukio hilo alilofanya ambalo halikuwa la kiungwana

“Bro Feisal najua tumeongea leo lakini naomba nikuombe radhi tena mbele ya mashabiki wa mpira”

banner

“Mpira ni burudani na sio uadui. Forgive me bro!,” ameandika Chama kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

Kuomba radhi ni kutambua kosa na kulijutia hivyo bila shaka Fei Toto pamoja na mashabiki wa Yanga, wadau wa soka wamemsamehe

Hata hivyo huenda akakabiliwa na hatua za kinidhamu kutoka kwa shirikisho la Mpira nchini (TFF)

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited