Home Soka Kagere Amaliza Mchezo

Kagere Amaliza Mchezo

by Sports Leo
0 comments

Ni Meddie Kagere ndiye aliyemaliza mchezo kati ya Simba sc na Azam baada ya kufunga bao pekee lililohakikisha msimbazi wanachukua pointi tatu muhimu kutoka chamazi.

Goli hilo alilofunga kwa kichwa baada ya kupokea pasi safi ya mbali kutoka kwa Francis Kahata na kupiga kichwa kilimuacha kipa Mwadini Ally akiruka bila mafanikio na kuwaacha mashabiki wa Azam fc wakiduwaa.

banner

Mchezo huo ulitawaliwa na rafu pamoja na matumizi ya nguvu na kufanya zaidi ya wachezaji watano wa Azam kupewa kadi za njano hasa katika kipindi cha kwanza huku Mzamiru Yassin akiwa ndie mchezaji aliyechezewa faulo nyingi zaidi.

Kwa ushindi huo Simba sc inakuwa imefikisha pointi 15 baada ya kucheza michezo 5 huku Meddie Kagere akiongoza safu ya wafungaji baada ya kufikisha mabao saba.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited