Kipa namba moja wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Aishi Manula ameongeza mkataba mpya wa miaka mitatu na klabu yake ya sasa ya Simba Sports Club yenye makao makuu msimbazi jijini Dar es salaam.
Manula aliyetokea Azam Fc ambayo ilimkuza kisoka baada ya kutumikia kikosi cha timu pili cha timu hiyo(timu ya vijana) na baadaye kupandishwa kikosi cha wakubwa na kufanikiwa kumvua namba mkongwe Mwadini Ally na kisha kuondoka kwa wanalambalamba wa chamazi miaka miwili iliyopita na kujiunga na Simba sc.
Hivi sasa manula ni miongoni wa wachezaji wenye mafanikio kikosini hapo akifanikiwa kuwapa taji la ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara kwa mara ya pili mfululizo huku akifanikiwa kuchukua tuzo ya kipa bora wa timu hiyo kwa mara ya pili mfululizo.,
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.