Home Soka Mbombo Nje Wiki 3

Mbombo Nje Wiki 3

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji wa klabu ya Azam Fc raia wa Congo DRC Idrissu Mbombo anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu baada ya kubainika kuwa anasumbuliwa na majeraha ya mguu aliyoyapata katika mchezo dhidi ya Mashujaa Fc uliofanyika mkoani Kigoma Novemba mosi mwaka huu.

Staa huyo alionekana kuimarika baada ya kupata maumivu hayo ambayo kwa wakati huo hayakua serious lakini sasa anapaswa kupata matibabu zaidi baada ya vipimo kuonyesha kuwa ana shida kubwa katika mguu wake.

“Baada ya hapo aliendelea vizuri na programu za mazoezi na wachezaji wenzake ila alijitonesha tena sehemu ya goti lake wakati wa mchezo na Ihefu kule Mbeya hivyo tulimfanyia vipimo na kugundua ni jeraha ambalo ni siriasi kidogo,” alisema Mbaruku Mlinga ambaye ni Daktari wa klabu hiyo.

banner

Mlinga aliongeza baada ya vipimo vya awali imegundulika atakuwa nje kwa wiki tatu huku akiwa kwenye uangalizi mzuri wa madaktari.

Mbombo amekua mchezaji tegemeo katika eneo la ushambuliaji la klabu hiyo tangu asajili akitokea El Gouna Fc ya nchini Misri Julai 2021.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited