Home Soka Mcolombia Fasta Atua Zenji

Mcolombia Fasta Atua Zenji

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji mpya wa Azam FC, Franklin Navarro (kulia) raia wa Columbia amewasilini kisiwani Unguja, Zanzibar na kukutana na kocha mkuu wa timu hiyo, Youssouph Dabo kwa ajili ya utambulisho na kufahamu zaidi kuhusu malengo ya timu hiyo msimu huu.

Azam FC ipo kisiwani humo kushiriki michuano ya Mapinduzi Cup ambayo ipo hatua ya makundi ikiwa tayari imecheza mchezo mmoja dhidi ya Mlandege Fc katika kundi A la michuano hiyo inayofuatliwa zaidi hapa nchini katika kipindi hiki cha  mwisho wa mwaka.

Staa ambaye ni raia wa kwanza wa Colombia kucheza katika ligi kuu ya NBC hapa nchini inatajwa kuwa atalipwa mshahara zaidi ya shilingi za kitanzania milioni 40 kwa mwezi katika mkataba wake aliousaini na mabosi wa klabu hiyo akizidiwa na Ali Ahmada ambaye analipwa takribani milioni 55 kwa mwezi.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited