Home Soka Mwigulu Atimiza Ahadi Yanga

Mwigulu Atimiza Ahadi Yanga

by Sports Leo
0 comments

Mbunge na mshabiki wa Yanga Mwigulu Nchemba tayari amekamilisha ahadi yake aliyoitoa mbele ya hadhira siku ya tamasha la kuichangia klabu hiyo ‘Kubwa kuliko’ lililofanyika katikati ya mwezi mei mwaka huu.

Katika tamasha hilo Mheshimiwa huyo ambaye alikua waziri wa mambo ya ndani miezi kadhaa iliyopita aliahidi kuichangia klabu hiyo kwa kusajili mchezaji mmoja kwa gharama zake mfukoni kama mchango wake kwa klabu hiyo.

Imebainika kuwa Mwigulu tayari ameshamalizana na mchezaji beki Ally Mtoni Sonso ambaye yupo nchini Misri na timu ya taifa ya Tanzania (Taifa stars) baada ya kumtuma mbunge mmoja kati ya wabunge waliokwenda nchini humo kuishangilia timu ya taifa ilipocheza na Senegali kwenda kukamilisha mazungumzo na mchezaji huyo.

banner

Kwa hali ilivyo mazungumzo yamefikia hatua za mwisho na tayari uongozi wa Yanga umeshawasili nchini Misri kwenda kumsainisha mchezaji huyo ili kuwahi kutuma majina ya usajili Caf ambapo mwisho ni june 30 mwezi huu kwa usajili wa kimataifa.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited