Home Soka Okrah Anarejea Soon

Okrah Anarejea Soon

by Sports Leo
0 comments

Usajili mpya wa klabu ya Yanga sc Augustine Okrah anatarajiwa kurejea katika mazoezi ya klabu hiyo muda mfupi ujao baada ya kuumia katika mchezo wake wa kwanza klabuni hapo dhidi ya Kvz katika kombe la Mapinduzi inayoendelea nchini Visiwani Zanzibar.

Okrah aliingia kwa mara ya kwanza uwanjani kuitumikia Yanga sc lakini ilipotimu dakika ya 57 ya mchezo aliumia baada ya kugongana vichwa na mchezaji wa Kvz na kuanza kutoka na damu puani hali iliyolazimika kukimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi ambapo kwa mujibu wa dakatari wa Yanga sc Moses Etutu ni kuwa anaendelea vizuri.

“aliumia jana wakati wa mechi yetu akapata head injury na akaanza kutoka na damu puani na baada ya kumpa huduma ya kwanza tulimkimbiza hospitali kwa matibabu zaidi ambapo baada ya vipimo tukabaini kwamba amevunjika baadhi ya mifupa ya kwenye pua kwa hiyo alipatiwa matibabu na mpaka sasa kiafya yuko stable na tunatarajia mpaka kesho anaweza kurejea nyumbani”Alisema Moses Etutu Daktari wa klabu hiyo

banner

Yanga sc imefanya usajili wa dirisha dogo ikilega kuboresha kikosi hicho kwenye michuano ya kimataifa ambapo mbali na Shekhan Ibrahim pia kikosi hicho kimemuongeza Okrah ambaye alikua ni mchezaji wa Simba sc mpaka alipotemwa na kujiunga na Benchem United ya nyumbani kwa Ghana.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited