Home Soka Samatta Atimiza Ndoto

Samatta Atimiza Ndoto

by Sports Leo
0 comments

Nahodha wa taifa stars Mbwana Samatta ametimiza ndoto yake ya kuifunga klabu ya Liverpool baada ya jana kufunga goli la kusawazisha dakika ya 40 ya mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya mchezo uliofanyika katika uwanja wa Anfield jana.

Liverpool walitangulia kupata goli kupitia kwa Georgio Wijnaldum ambalo lilisawazishwa na staa huyo kabla ya Alex-Oxlade Chamberlain kuongeza bao la pili na la mwisho kufanya liverpool kuongoza kundi E.

Samatta aliweka ahadi ya kuifunga Liverpool katika mchezo wa marudiano baada ya kupata uzoefu katika mchezo wa kwanza ambapo alikabiliana na beki mahiri Virgil Van Djik.

banner

“Najivunia wachezaji wangu,tumecheza kamari kucheza na timu bora duniani hakika tumefanya vizuri”Alisema kocha wa Genk Felice Mazzu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited