Home Soka Sikukurupuka-Ajibu

Sikukurupuka-Ajibu

by Sports Leo
0 comments

Staa wa klabu ya Simba sc Ibrahim Ajibu Migomba amesema kuwa hakukurupuka kujiunga na klabu ya Simba sc na kukataa ofa nono ya klabu ya Tp Mazembe ya Lububumbashi nchini Congo.

Staa huyo aliyewika akiwa na klabu ya Yanga kiasi cha kuwavutia matajiri hao wa madini kutoka Congo alisema hayo wakati akihojiwa na mwandishi mwandamizi Shaffih Dauda.

Baada ya ofa kumfikia Ajibu anasema alikaa na familia yake akapata ushauri lakini pia alipata ushauri kutoka kwa nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta halafu yeye akafanya maamuzi ya mwisho kwa kuzingatia ushauri aliopata kwa watu wote.

banner

Akizungumza na Shaffihdauda amejibu anasema Samatta alimwambia aende sehemu ambayo atakuwa na furaha na itakuwa na manufaa kwa familia yake.

Baada ya ushauri huo ndipo alipofikiria na kuamua kujiunga na klabu ya Simba akiacha dola 50000 na mshahara wa dola 5000 aliowekewa na Tp Mazembe.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited