Home Soka Simba sc Yatoa Sare Morroco

Simba sc Yatoa Sare Morroco

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simbab sc imefanikiwa kupata sare ya mabao 1-1 dhidi ya klabu ya Olympique Club de Khouribga mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu na michuano ya kimataifa uliofanyika katika kambi ya klabu hiyo nchini Morroco.

Kocha Didier Gomes aliwaanzisha Ally Salim,Gadiel Michael,Henock Inonga,Pascal Wawa,Pape Osmane Sakho,Sadio Kanoute,Benard Morrison huku pia Hassan Dilunga,Rally Bwallya na Chris Mugalu katika kikosi cha kwanza ambapo kilipata bao la kuongoza kupitia kwa Pape dakika ya 37.

Kipindi cha pili dakika za mwishoni Olympique Club de Khouribga walisawazisha na kufanya mchezo umalizike kwa suluhu huku makocha wa timu zote wakionekana kuwa bize na maandalizi ya vikosi vyao.

banner

Huu ni mchezo wa pili wa kirafiki kwa klabu ya Simba sc ambapo mchezo wa awali walicheza na Far Rabat na kutoa sare ya mabao 2-2 huku kikosi hicho kikitarajiwa kurejea nchini wikiendi hii.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited