Home Soka Tetesi Za Usajili Ulaya

Tetesi Za Usajili Ulaya

by Sports Leo
0 comments

Manchester United ianajiandaa kutangaza dau la kumnunua mlinzi wa Juventus na Uholanzi Matthijs de Ligt, 20, huku kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 27, akiwa tayari kuondoka Old Trafford. (Star)

Man U hueda ikalazimika kumlipa mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez, 31, ada ya kila mwaka ya £1.1m atakaporejea kutoka Inter Milan ambako amekuwa akicheza kwa mkopo. (Sun)

Everton inapanga kuweka dau kubwa la kumnunua mshambuliaji wa Real Madrid na Wales Gareth Bale, 30, msimu wa joto pamoja na kiungo wa kati wa Juventus Aaron Ramsey, 29. (90min.com)

banner

Kwa sasa, the Toffees wanatumia huduma ya mawasiliano ya kidigitali ya Zoom inayowakutanisha kwa njia ya video wachezaji na wahudumu wa afya wa klabu hiyo, huku kiungo wa kati wa Ufaransa aliyejeruhiwa Schneiderlin, 30, akijiandaa kuzungumza na mtaalamu wake wa upasuaji kupitia mfumo huo. (Guardian)

Mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema, 32, ametetea kauli yake baada ya kumfananisha mshambuliaji wa Chelsea na mchezaji mwenza wa timu ya taifa ya Ufaransa Olivier Giroud, 33, ‘gari dogo linaloenda kasi lakini halina nguvu’alipofanya Instagram live. (Marca)

Arsenal inawataka ndugu wawili wa Ivory Coast, Hamed Traore, 20, kiungo wa kati ambaye yuko Sassuolo kwa mkopo kutoka Empoli, na ndugu yake Amad, 17, ambaye ni winga wa Atalanta. (90min.com)

Liverpool haina mpango wa kumsajili tena kiungo wa kati wa Brazil Philippe Coutinho, 27, ambaye yuko Bayern Munich kwa mkopo kutoka Barcelona huku Mamchester United ikisemekana kumvutia kasi. (Mirror)

Manchester United imeelekeza darubini yao kwa kiungo wa kati wa Leicester City na England James Maddison, 23, baada ya nahodha wa Aston Villa Jack Grealish, 24, ambaye wamekuwa wakimnyatia kwa muda mrefu (Mirror)

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited