Home Soka Tshabalala Asaini Simba

Tshabalala Asaini Simba

by Sports Leo
0 comments

Beki wa kushoto wa Simba sc Mohamed Hussein Zimbwe JR amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kusalia klabuni hapo baada ya ule wa awali kufikia tamati msimu huu.

Beki huyo amesaini kandarasi hiyo yenye thamani ya mamilioni akifata nyayo za wenzake John Bocco,Meddie Kagere,Jonas Mkude na wengine ambao wote wameamua kusalia klabuni hapo kufuatia kuwa na misimu miwili yenye mafanikio kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu bara mara mbili mfululizo na kufika hatua ya robo fainali katika ligi ya mabingwa barani Afrika.

Zimbwe Jr alijiunga na Simba akitokea katika klabu ya Kagera Sugar na toka amejiunga klabuni hapo miaka kadhaa iliyopita amejihakikishia nafasi katika upande wa beki wa kushoto wa Timu hiyo.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited