Home Soka Usajili mpya Yanga kuonekana Mapinduzi cup

Usajili mpya Yanga kuonekana Mapinduzi cup

by Sports Leo
0 comments

Uongozi wa klabu ya Yanga umeweka wazi kuwa majembe mapya yaliyosajiliwa na klabu hiyo kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili yataanza kuonekana rasmi kwenye michuano ya Mapinduzi cup inayotarajiwa kuanza hivi karibuni huko Zanzibar.

Yanga inatajwa kukamilisha usajili wa kiungo wa Azam FC Sure Boy,winga wa Biashara United Denis Nkane na golikipa wa Mtibwa Sugar Aboutwalib Mshery kukiongezea nguvu kikosi hiko kwenye harakati zake za kupigania ubingwa ligi kuu soka Tanzania Bara.

Mshery anatajwa kwenda kuchukua nafasi ya Ramadhan Kabwili anayesemekana kuachwa na klabu hiyo,usajili huu pia utakuwa muhimu kwa Yanga hasa ukizingatia muda si mrefu itampoteza golikipa wake namba moja Djigui Diarra atakayekwenda kuitumikia timu yake ya taifa ya Mali kwenye michuano ya AFCON mwezi Januari huko Cameroon.

banner

Afisa habri wa klabu hiyo Hasan Bumbuli alisema kuwa timu hiyo itafanya usajili wa wachezaji mkupitia dirisha hili dogo ambapo katika usajili huo wapo ambao watatumika katika michuano ya Mapinduzi na wengine hawatatumika kulingana na matakwa ya timu.

Yanga imerejea Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Biashara United Disemba 26 siku ya boxing day.kisha wataelekea Zanzibar kutetea ubingwa wao wa kombe la Mapinduzi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited