Home Soka Yanga Kuivaa Pamba Jumamosi

Yanga Kuivaa Pamba Jumamosi

by Sports Leo
0 comments

Timu ya Yanga sc imeweka kambi jijini Mwanza kujiandaa na mechi ya kimataifa kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika ambapo timu hiyo itacheza mchezo wa kirafiki na Pamba fc ya jijini humo.

Yanga imeamua kuweka kambi jijini humo baada ya kuombwa na uongozi wa matawi ya timu hiyo jijini humo ambao pia umegharamia safari na kambi hiyo.

Licha ya kucheza mchezo wa kirafiki pia timu hiyo itajitolea kuchangia damu katika hospitali ya Sokoetoure iliyopo jijini humo siku ya asubuhi kabla ya mchezo.

banner

Yanga itavaana na Zesco tarehe 14 septemba nchini Zambia kabla ya marejeano kufanyika jijini Dar es salaam wiki mbili badae.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited