Home Soka Yao Kouasi Amponza Jeremia Juma

Yao Kouasi Amponza Jeremia Juma

by Sports Leo
0 comments

Nyota wa Tanzania Prisons Jeremia Juma amekumbana na adhabu ya kufungiwa michezo mitatu na kupigwa faini ya shilingi milioni moja baada ya kumkanyaga nyota wa Yanga Yao kouassi kwenye mechi ambayo Prisons ilipoteza kwakufungwa magoli 2-1 iliyofanyika siku ya Jumapili Februari 11.

Adhabu hiyo imetolewa na bodi ya ligi kuu nchini baada ya kufanya kikao cha tathmini ya mechi za ligi kuu siku ya Februari 14 ambapo Juma amepewa adhabu hiyo kwa mujibu wa kanuni namba 41:5 kuhusu udhibiti wa mchezo.

Jeremia Juma alimkanyaga beki huyo dakika ya 52 ya mchezo ambapo mwamuzi Ahmed Arajiga hakuliona tukio hilo kutokana na kuwa mbali japo kamisaa wa mchezo huo alifanikiwa kuliona na kuliandika katika ripoti ya mchezo huo.

banner

Kouasi amekua na kiwango kizuri tangu atue Yanga sc ambapo pia katika mchezo huo alitoa pasi ya bao  la kwanza kwa Clement Mzize na kufikisha jumla ya asista sita msimu huu.
.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited