Home Makala Aucho Fiti Kuivaa Azam Fc

Aucho Fiti Kuivaa Azam Fc

by Sports Leo
0 comments

Kiungo wa klabu ya Yanga sc Khalid Aucho amepona majearaha yake na sasa ataungana na timu yake katika maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc utakaofanyika katika uwanja wa Chamazi April 6.

Aucho alikua anasumbuliwa na maumivu ya misuli yaliyopelekea kuikosa michezo dhidi ya Geita Gold na Kmc licha ya klabu yake kuibuka na ushindi lakini pengo lake katika kulimiliki dimba lilionekana.

Akizungumzia hali ya Aucho, Mtaalamu wa Viungo na Daktari wa Yanga, Youssef Mohammed, amesema: “Kuhusu hali ya Aucho mashabiki wa Yanga hawapaswi kuwa na wasiwasi kwani tayari ameshapona kwa asilimia 100 ndiyo maana aliruhusiwa kujiunga na kikosi cha Timu ya Taifa ya Uganda.

banner

“Akirejea ataungana na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Azam FC,”Alisema daktari huyo kipenzi cha wachezaji wa klabu hiyo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited