Home Soka Gadiel Atua South Afrika

Gadiel Atua South Afrika

by Sports Leo
0 comments

Mchezaji na nahodha wa klabu ya Singida Fountain Gate Fc Gadiel Michael amejiunga na timu ya Cape Town Spurs Fc kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya timu hizo kufika makubaliano ya kufanya biashara ya mchezaji huyo.

Gadiel mchezaji wa zamani wa Azam Fc,Yanga sc na kisha Simba sc anaondoka nchini mchana wa leo kwenda nchini humo kukamilisha dili hilo la kujiunga na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Afrika ya kusini.

“Gadiel Michael anaenda kujiunga na Cape Town Stars ya Afrika Kusini na anatarajia kuondoka leo”.Alisema Rais wa Singida Fountain Gate Japhet Makau wakati wa mkutano na waandishi wa habari mchana wa leo akielezea hali ngumu ya kifedha ambayo klabu hiyo inapitia.

banner

Mbali na Gadiel Michael klabu hiyo pia imeachana na mastaa wake wengine kama Elvis Rupia,Abubakar Khomein,Duke Abuya,Joash Onyango na Mauruf Tchakei ili kubana matumizi kutokana na hali mbaya kifedha.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited