Home Soka Onana,Lakred Kuwakosa Asec

Onana,Lakred Kuwakosa Asec

by Sports Leo
0 comments

Mastaa wa klabu ya Simba sc Willy Esomba Onana na kipa Ayoub Lakred wanatarajiwa kuukosa mchezo wa ligi ya mabingwa hatua ya makundi dhidi ya Asec Mimosa utakaofanyika nchini Ivory Coast siku ya ijumaa Februari 23 baada ya kuwa na sababu mbalimbali ikiwemo majeraha na kadi za njano.

Onana ataukosa mchezo huo kutokana na kusumbuliwa na majeraha ambapo pia John Bocco naye ataukosa kutokana na sababu hiyo hiyo huku kipa Ayoub Lakred ambaye ameibuka kuwa muhimu kikosini humo siku za karibuni nae ataukosa mchezo huo kutokana na kuwa na kadi tatu za njano.

Onana na Bocco siku za karibuni wamekua sio pengo sana kikosini humo kutokana na kuwa na mbadala sahihi kikosini humo huku Lakred akitarajiwa kuwa pengo kutokana na umuhimu wake hasa uzoefu wa michuano ya kimataifa ambapo amekua akifanya vizuri japo uwepo wa kipa Aishi Manula utaleta nafuu zaidi.

banner

Simba sc inatarajiwa kusafiri siku ya kesho alfajiri kuelekea nchini humo kusaka alama tatu ambazo zitawasaidia kupata alama za kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya klabu bingwa.

Mpaka sasa katika msimamo wa kundi B Asec Mimosa yupo kileleni akiwa na alama 10 huku Simba sc ikiwa katika nafasi ya pili ya msimamo ikiwa na alama 5 baada ya timu zote kucheza michezo minne.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited