Home Soka Simba Sc Kumaliza Kazi Dar

Simba Sc Kumaliza Kazi Dar

by Sports Leo
0 comments

Baada ya kutoka suluhu nchini Ivory Coast katika mchezo wa klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Asec Mimosa sasa klabu ya Simba sc inajipanga kuja kumaliza kazi kwa ushindi mnono ili kufuzu robo fainali ya michuano hiyo katika mchezo dhidi ya Janweng Galax utakaofanyika Machi  2 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Simba sc baada ya kumaliza kwa matokeo ya 0-0 nchini Ivory Coast sasa msimamo wa kundi hilo la B ni tayari Asec Mimosa amefuzu akiwa na alama 11 huku Simba sc akiwa na alama 6 katika ya pili ya msimamo huku Janweng akiwa na alama tano na Wydad AC wakiwa na alama nne.

Endapo Simba sc watashinda mchezo huo basi watafikisha alama tisa ambazo moja kwa moja zitawafanya kufuzu hatua ya rob0 fainali baada ya kushindwa misimu kadhaa nyumba kufuzu tangu walipotolewa na Tp Mazembe msimu wa 2018/2019 katika hatua ya robo fainali.

banner

Pengine habari ingekua nyingine kama Simba sc wangetumia vyema nafasi kadhaa walizopata katika mchezo huo hasa ile ya mapema kipindi cha pili ambayo Sadio Kanoute alikosa akiwa yeye na goli.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited