Home Soka Phiri Atua Dynamos

Phiri Atua Dynamos

by Sports Leo
0 comments

Aliyekua mshambuliaji wa klabu ya Simba Sc Moses Phiri amejiunga na Power Dynamos ya Zambia kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kumalizana na klabu ya Simba sc aliyoitumikia kwa misimu miwili kabla ya kocha Abdelhack Benchika kuamua kuachana nae.

Mshambuliaji huyo alikuwa akiichezea timu hiyo aliyojiunga nayo kwa mkopo Januari 16, mwaka huu akitokea Simba, baada ya kutokuwa na nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza hivyo kuamua kutafuta changamoto sehemu nyingine.

Kwa mujibu wa mchezaji huyo wa zamani wa Zanaco Fc kulikua na ofa nyingine lakini aliamua kumalizana na Power Dynamos kutokana na kufikia makubaliano mazuri kuliko klabu nyingine za ndani na nje ya Zambia.

banner

Tayari staa huyo ameshajiunga na kambi ya maandalizi ya msimu mpya nchini humo iliyoko Lusaka Zambia huku akitarajiwa kurejesha makali yake yaliyoifanya Simba Sc kuamua kuvunja benki kumnasa na kuwazidi ujanja Yanga sc.

Msimu wake wa kwanza mwaka 2022 alipotua Simba sc alifunga jumla ya mabao kumi nyumba na Saido Ntibanzokiza aliyefunga mabao 17 sambamba na Fiston Kalala Mayele huku msimu wa pili kutokana na majeraha alifunga mabao matatu pekee japo aliondoka katikati ya msimu.

 

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited