Home Soka Azam Fc Yatinga Fainali Ngao ya Jamii

Azam Fc Yatinga Fainali Ngao ya Jamii

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Azam Fc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la ngao ya jamii uliofanyika katika uwanja wa New Amaan complex Visiwani Zanzibar.

Katika mchezo Azam Fc ilianza kupata bao la mapema dakika ya 10 kupitia kwa Gibril Sillah aliyepiga shuti kali baada ya kupokea pasi ya Feisal Salum dakika ya 13 ya mchezo.

Bao hilo halikudumu sana baada ya Abdalah Semfuko kusawazisha kwa kichwa dakika ya 27 huku Feisal Salum akiongeza bao la pili kwa Azam Fc kwa shuti kali dakika ya 40 na dakika chache kabla ya mapumziko Jhonier Blanco alifunga bao la tatu kwa Azam Fc kwa kichwa akiunganisha krosi ya Lusajo Mwaikenda.

banner

Kipindi cha pili kilianza taratibu mpaka dakika ya 86 ambapo Coastal walipata bao la pili kupitia kwa Hassan lakini walikosa umakini na kuruhusu mabao mawili ya haraka kwa Azam Fc kupitia kwa Adam Adam dakika ya 87 na Ever Meza dakika ya 90+2 ya mchezo.

Azam Fc sasa itarejea Dar es salaam kucheza na Yanga sc katika mchezo wa fainali siku ya Jumapili August 11 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited