Home Soka Caf Yazipa Mamilioni Yanga Sc,Azam Fc

Caf Yazipa Mamilioni Yanga Sc,Azam Fc

by Sports Leo
0 comments

Shirikisho la Soka barani Afrika (Caf) limetoa mgawo wa fedha dola elfu hamsini kwa klabu zote zinazoshiriki michuano ya klabu bingwa barani Afrika na Kombe la Shirikisho katika hatua ya awali.

Fedha hizo zilikua hazitolewa hapo nyuma ambapo klabu zililazimika kujigharamia kila kitu katika hatua za awali lakini msimj huu Caf chini ya Rais wa Shirikisho hilo Patrice Motsepe imeamua kuvipa fedha hizo vilabu vyote vinavyoshiriki hatua hiyo.

Kwa Tanzania vilabu vya Yanga sc ambayo itavaana na Vital O ya Burundi sambamba na Azam Fc itakayovaana na Apr ya Rwanda na Coastal union vitapata mgao huo.

banner

Vilabu ambavyo vitafuzu hatua ya makundi vitapata tena mgawo kutoka Caf na utakua unaongezeka kila hatua huku mshindi wa kombe la klabu bingwa akiwa na uhakika wa kupata zaidi ya dola milioni nne na wa kombe la Shirikisho atajipatia dola milioni mbili na nusu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited