Klabu ya Kmc imekamilisha usajili wa Kocha wa zamani wa klabu ya Azam Fc Kally Ongara akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Kocha Abdulhamid Moalin ambaye amejiuru siku chache zilizopita.
Kally ametambulishwa rasmi mbele ya waandishi wa habari mapema hii leo ambapo atakua na jukumu la kuhakikisha anairudishia Kmc makali yake katika ligi kuu ya Nbc nchini.
Kally ambaye amewahi kuifundisha Azam Fc kwa nyakati tofauti tofauti amesaini mkataba huo mbele ya Meya wa Halmashauri ya Kinondoni ndugu Songoro Mnyonge na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi Hanifa Selemani.
Mkataba huo haujawekwa wazi utakua wa muda gani na huku taarifa zikisema kuwa Kmc imeamua kumuajiri kocha huyo kutokana na kuridhika na falsafa zake ambapo mabosi hao pamoja na kuwa na rundo la Cv waliamua kumchagua kocha huyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini mpaka sasa Kmc imevuna alama 14 ikicheza michezo 11 ya ligi kuu huku ikiwa na wastani wa -3 wa mabao ya kushinda na kufungwa.