Home Makala Orlando Pirates Yatua Kwa Fadlu Davis

Orlando Pirates Yatua Kwa Fadlu Davis

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini imehamia kwa kocha wa klabu ya Simba Sc Fadlu Davis Baada ya kuambiwa kuwa José Luis Riveiro hatokuwa sehemu ya benchi la ufundi kuelekea msimu ujao.

Fadlu aliwahi kuifundisha klabu hiyo kama kocha msaidizi na sasa klabu hiyo imefanya jitihada za kumrudisha ambazo mpaka sasa zimegonga mwamba baada ya kocha huyo kugomea dili hilo.

banner

Mbali na klabu hiyo pia klabu ya Raja Club Athletic kutoka Morocco na wao walifika mezani kwa Fadlu Davids lakini mtaalamu huyo  akawajibu kuwa hayupo tayari kwa sasa.

“Sipo tayari kuondoka kwa sasa na natamani nifanikiwe zaidi nikiwa hapa Simba Sc” Alisema kocha huyo baada ya kuulizwa kuhusu ofa hizo zilizofika mezani kwake.

Fadlu amevivutia vilabu hivyo kutokana na kuifanya Simba sc kuwa tishio ndani ya muda mfupi tangu ajiunge nayo akichukua nafasi ya Roberto Oliveira “Robertinho” aliyetimuliwa klabuni hapo baada ya kufungwa 5-1 na Yanga sc.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited