Home Makala Fifa Kufanya Ukaguzi TFF

Fifa Kufanya Ukaguzi TFF

by Sports Leo
0 comments

Shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA) linatarajia Kufanya uchunguzi wa mpira wa Tanzania katika Kipindi cha miezi miwili nyuma hadi sasa kutokana na migogoro ya kimaamuzi iliyotokea.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani ni kuwa  kamati ya nidhamu FIFA ilituma barua kwenda TFF mnamo Juni 13, 2025 ikiwataarifu kuwa inafuatilia mienendo ya soka la Tanzania ikiwa ni pamoja viashiria vya siasa kuingilia masuala ya soka.

Aidha FIFA imeitaka TFF kutoa ushirikiano katika uchunguzi wao huo hatua inayokuja kufuatia sintofahamu iliyotokea kwenye soka la Tanzania kwa kipindi cha miezi mitatu tangu kuahirishwa kwa Derby ya Kariakoo mnamo Machi 8.

banner

Pamoja na Taarifa hiyo pia FIFA imeitaka TFF kutoa ushirikiano wa kutosha kwa maofisa wa FIFA watakaokuwepo nchini kwa ajili ya ukaguzi huo ambapo pia watakagua masuala ya fedha na maamuzi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited