250m Kumpata Yakoub wa Jkt Tanzania

Screenshot 20250629 171441 Instagram

Kiasi cha Shilingi 250m Kumpata Yakoub Seleman wa Jkt Tanzania ikiwa ni ada ya usajili ili kumuachia golikipa wao Yakoub Suleiman (25) ambaye anatakiwa na klabu ya Simba Sc msimu ujao.

Simba Sc tayari imewasiliana na JKT Tanzania ikitaka saini ya kipa huyo ambaye alikuwa na msimu bora akimaliza na clean sheet nane katika ligi kuu msimu huu na mazungumzo yameanza baina ya timu hizo.

Screenshot 20250629 171343 Instagram

Simba sc inahitaji sana huduma ya golikipa huyo kuelekea msimu ujao kwa ajili ya kutoa ushindani kwa Moussa Camara na tayari imempoteza kipa Aishi Manula aliyejiunga na Azam Fc na sasa mchakato umeanza na mazungumzo yanaendelea vizuri sana baina ya pande zote mbili

Simba sc itaachana na kipa Hussein Abel ambaye ameshindwa kuwashawishi mabosi wa klabu hiyo na sasa inaingia sokoni kumsaka mrithi wake.

Kwenye mechi 21 za ligi kuu akiwa na JKT,Yakubu Suleimani ameweza kuondoka na clean sheets 8,alikuwa na msimu mzuri mpaka ikamfanya aitwe kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania “Taifa Stars”.

 

Leave a Reply

Enable Notifications OK No thanks