Adebayor Aondoka Singida Black Stars

Nyota wa kimataifa wa Niger Victorien Adebayor Aondoka Singida Black Stars ambapo sasa ameachana rasmi na klabu hiyo baada ya kuhudumu kikosini hapo kwa msimu mmoja tu tangu ajiunge na kikosi hicho.
Nyota huyo (28) hakuwa na msimu mzuri ndani ya kikosi cha Singida msimu uliopita ambapo amekua chaguo la tatu nyuma ya Jonathan Sowah na mshambuliaji raia wa Kenya Elvis Rupia ambao wamekua wakianza mara kwa mara.
Hata hivyo tangu aondoke Us Gendarmerie ya nyumbani kwa Niger staa huyo amekua na kiwango ch kusuasua mara kwa mara huku majeraha nayo yakimuandama mara kadhaa.
Uongozi wa Singida Black Stars umeona ni vyema kuachana na mshambuliaji huyo ili kusajili mshambuliaji mwingine atakayekua na mchango mkubwa katika eneo la ushambuliaji la klabu hiyo.
Mpaka sasa Black Stars inaweza kuachana na mastaa wengine kama Arthur Badda na Marouf Tchakei ambao wana ofa nje ya nchi huku Edmund John akiwa naye ana ofa ndani ya nchi.
