Timu ya soka ya Tanzania(Taifa stars) inatarajiwa kuingia kambini siku ya jumapili ili kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani(Chan) zitakazofanyika nchini Cameroon Mwaka 2020.
Mchezo huo dhidi ya Sudan utafanyika mjini Kigali nchini Rwanda baada ya wenyeji kuchagua nchi hiyo baada ya Caf kuzuia mchezo huo kufanyika nchini Sudan kusini kwa sababu za kiusalama kisha marudiano yatafanyika nchini baada ya wiki mbili toka mchezo wa kwanza.
Tanzania imepata nafasi hiyo ya kucheza mechi hiyo baada ya kufanikiwa kuitoa Kenya kwa mikwaju ya penati mjini Nairobi baada ya awali kutoka sare ya 0-0 jijini Dar es salaam.