Diarra Akabidhi Jezi ya Aucho Yanga Sc

Rasmi Lassine Kouma raia wa Mali amesaini Yanga Sc Lassine Kouma amepewa Jezi namba 8 aliyokuwa anavaa Khalid Aucho akitokea klabu ya Stade de Malien ya nchini Mali.
Kwa mujibu wa Kouma ni kuwa kipa wa Yanga sc Djigui Diarra ndiye aliyefanya kazi kubwa kumshwishi staa huyo kuacha ofa za ulaya na kujiunga na Yanga sc baada ya kumuelezea kuhusu uzuri wa maisha ya Yanga sc.

“Kwanza namshukuru Mungu nimeifuatilia Yanga Sc tangu Djigui Diarra alipofika hapa ila pia niliwafuatilia walivyokuja Mali kucheza dhidi ya Real Bamako niliona namna Diarra alivyokuwa na furaha lakini pia jinsi timu ilivyokuwa imejipanga hivyo toka kipindi hicho nilikuwa na shauku ya kuchezea hapa siku Moja maana nilikuwa kama Shabiki toka nimewajua nina furaha sana kuwa hapa”,Alisema kiungo huyo kinda
“Nilifurahi sana na kujivunia kusikia Yanga inataka kunisajili ili nije kucheza hapa, hivyo nina furaha sana, Djigui Diarra aliniambia Yanga ni timu nzuri na ni klabu kubwa sana na mengine mengi ila alinieleza kuhusu ukuwa wa hii klabu”,Alimalizia kusema kwa furaha.
Kouma ambaye pia alikua anaviziwa na klabu za Al Hilal Fc na Simba ambazo zote alikataa ofa zao akisubiri ofa ya Yanga sc ambapo baada ya Viongozi wa Yanga sc kujiridhisha kuhusu ubora wa kiungo huyo walipiga simu moja na kumaliza dili hilo.
Kouma amepewa jezi namba nane iliyokua ikivaliwa na Khalid Aucho kikosini humo ambapo ana uwezo wa kucheza nafasi zote na kiungo mshambuliaji wa kati ama wa pembeni.
