Klabu ya As Vita imenyang’anywa ubingwa wa ligi kuu nchini Congo baada ya kupokonywa pointi tisa kwenye ligi kuu sawa na michezo (3) ambayo walimchezesha mchezaji Zao Matutala ambaye alikua amefungiwa.
Mchezaji huyo Zao Matutala ambaye kwa sasa amefungiwa amefungiwa miezi (12) kujihusisha na soka alikuwa na kesi kipindi anachezeshwa na As Vita ambapo kesi ilikua katika mahakama ya michezo ya kimataifa(Cas) na sasa baada ya majibu kutoka amekutwa na hatia hivyo mechi zote tatu walizomchezesha wamenyang’anywa points.