Home Soka Aziz Ki,Feisal Mwisho wa Ubishi

Aziz Ki,Feisal Mwisho wa Ubishi

by Sports Leo
0 comments

Leo ndio mwisho wa ubishi wa nani anastahili tuzo ya mchezaji bora na kiungo bora wa msimu uliopita wa ligi kuu nchini baina ya Feisal Salum wa Azam Fc na Stephane Aziz Ki wa Yanga sc katika usiku maalumu wa tuzo hizo utakaofanyika jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Super Dome Masaki.

Aziz Ki na Feisal wanawania tuzo hizo mbili ambazo zimezua mjadala mkubwa kwa mashabiki kuhusu nani anastahili  kupewa tuzo ya Mvp wa ligi kuu msimu uliopita ambapo Azizi Ki alimaliza mfungaji bora akiwa na mabao 21 na Feisal kumaliza katika nafasi ya pili akiwa na mabao 19 huku Aziz Ki akiwa na Assiti nane za mabao na Feisal Salum akiwa na assisti saba.

Mpaka sasa Aziz Ki ameshachukua tuzo ya mfungaji bora kutokana na kuwa na idadi ya mabao 21 ambayo hayajafikiwa na mchezaji yeyote hapa nchini kwa msimu uliopita huku kimuhemuhe kikibaki katika tuzo hizo mbili ambapo atakayechukua tuzo ya kiungo bora basi atakua na asilimia kubwa ya kuchukua na tuzo ya mchezaji bora wa mwaka.

banner

Msimu huu tayari mastaa hao walikua na timu zao katika kambi ya maandalizi nje ya nchi huku Feisal akiwa Morocco na Azam Fc na Azizi Ki akiwa Afrika ya Kusini na Yanga sc na tayari mastaa wote wamesharejea na wanatarajiwa kuwapo katika tuzo hizo usiku wa leo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited