Home Makala Chama,Mgunda Watwaa Tuzo

Chama,Mgunda Watwaa Tuzo

by Sports Leo
0 comments

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba sc Cletous Chama pamoja na kocha wake Juma Mgunda kwa pamoja wametwaa tuzo ya mchezaji bora na kocha bora wa mwezi Disemba mwaka jana kwa mujibu wa kamati inayosimamia ligi kuu ya Bodi ya ligi kuu nchini (TPLB).

Taarifa iliyotolewa na bodi hiyo inasema kuwa Mgunda ametwaa tuzo hiyo akiwashinda makocha Nasreddine Nabi na Hans Van Pluijm wa Singida Big Stars ambapo Mgunda alifanikiwa kushinda mechi nne na kupata sare mchezo mmoja katika michezo mitano aliyiongoza timu hiyo katika ligi kuu nchini.

Kwa upande wa Chama yeye alifanikiwa kufunga mabao mawili na kusaidia upatikanaji wa mabao mengine matano katika michezo hiyo mitano ya ligi kuu akiwapiku Fiston Mayele na John Boko wa Simba sc.

banner

Mgunda anakua kocha wa kwanza msimu huu kutwaa tuzo hizo mara mbili mfululizo kwa msimu huu akitwaa tena tuzo hiyo mwezi Novemba mwaka huu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited