Home Makala Feisal Aweka Ngumu Yanga sc

Feisal Aweka Ngumu Yanga sc

by Sports Leo
0 comments

Pamoja na kwamba amewasilisha barua ya kutaka kuondoka klabuni hapo ikiwemo kulipa kiasi cha shilingi milioni 112 kama fidia ya kuvunja mkataba bafdo staa huyo amegoma kufanya mazungumzo ya aina yeyote na mabosi wa klabu hiyo ambao wamekua wakihaha kumtaka abadilishe mawazo.

Feisal tayari inasemekana ameshamwaga wino wa kuitumikia Azam Fc huku akipewa mshahara wa kiasi cha shilingi milioni 17 kwa mwezi ambao ni mara nne ya shilingi milioni nne anazolipwa sasa Yanga sc na tayari mpaka sasa hajalipoti kambini baada ya kutoweka siku chache zilizopita.

Feisal alisaini mkataba wa miaka minne ambao unapaswa kumalizika juni 30,2024 lakini ametumia mwanya huo kuvunja mkataba japo kumekua na sintofahamu endapo Yanga sc wakiamua kuchukua hatua zaidi za kisheria ambapo mpaka sasa inasemekana mabosi wa klabu hiyo tayari wamezirudisha fedha hizo pamoja na kumuandikia barua staa huyo aheshimu mkataba huku mamlaka kama Shirikisho la soka nchini pia likijulishwa.

banner

Viongozi kadhaa wa serikali ambao ni mashabiki wa klabu ya Yanga sc akiwemo Waziri wa fedha Mh.Mwigulu Nchemba na Ridhiwani Kikwete wamejaribu kumshawishi staa huyo lakini wameshindwa baada ya kuendelea kusimamia msimamo wake huo na mpaka sasa hajaripoti kambini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited