Home Makala Mashindano Ya Diplomatic Golf Kuanza Mei,30

Mashindano Ya Diplomatic Golf Kuanza Mei,30

by Sports Leo
0 comments

Mashindano ya Diplomatic Golf msimu wa pili yanayoratibiwa na kampuni ya Tanzania Mwandi kwa kushirikiana na wizara ya mambo ya nje ya nchi na ushirikiano wa Afrika Mashariki, yanatarajiwa kuanza Mei 30, 2020 viwanja vya Kilimanjaro Golf Club, Usa River jijini Arusha.

Maandalizi ya mashindano hayo ambayo yanafanyika kila mwaka yameendelea kwa nguvu leo Machi 17, 2020 Viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.

Akizungumza viwanjani hapo wakati wa maandalizi hayo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro amesema maadalizi hayo yanaendelea vizuri na kwa kiwango cha juu.

banner

“Diplomatic Golf ni fursa mahususi kwa mawaziri, wabunge, wanasiasa, wanadiplomasia na wananchi wote wa kawaida kukutana na kubadilishana uzoefu wa mchezo huo na kutengeneza njia mbadala ya kuikuza tasnia hiyo kwa kushirikiana na wadau wapenda golf, hivyo ninawasihi sote tujitokeze kwa wingi kushiriki mashindano haya,” alisema Ndumbaro.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited