Home Makala Mastaa Yanga Wakabidhiwa Tuzo

Mastaa Yanga Wakabidhiwa Tuzo

by Sports Leo
0 comments

Katika mchezo wa ligi kuu nchini baina ya Azam Fc dhidi ya Yanga sc mastaa wa Yanga sc pamoja na kocha Nasreddine Mohamed Nabi walikabidhiwa tuzo zao walizoshinda kama kocha na wachezaji bora wa mwezi wa ligi ambazo hutolewa na bodi ya ligi.

Tuzo hizo ambazo zimekabidhiwa ni Tuzo ya kocha bora na mchezaji bora ya mwezi wa kumi mwaka jana ambapo mshindi alikua Kocha Nabi na Feisal Salum huku tuzo ya mwezi januari ambapo k Fiston Kalala Mayele alishinda huku tuzo ya mwezi Februari ikienda kwa Nabi sambamba na Saido Ntibanzokiza.

Yanga sc imekua na mfululizo wa matokea mazuri kiasi cha mastaa wa klabu hiyo kutwaa tuzo za mwezi mara nyingi zaidi kushinda klabu yeyote nchini kwa msimu huu.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited