Home Makala Ntibanzokiza Akwama Geita Fc

Ntibanzokiza Akwama Geita Fc

by Sports Leo
0 comments

Kiungo mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Yanga sc Saido Ntibanzokiza amekwama kucheza katika michuano ya kimataifa akiwa na klabu yake mpya ya Geita Gold Fc baada ya usajili wake kutopitishwa na Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) kama moja ya wachezaji wa klabu hiyo katika michuano ya kombe la shirikisho.

Katika orodha iliyotolewa na Shirikisho la soka nchini imeonyesha wachezaji wote wa klabu hiyo lakini jina la staa huyo halimo kutokana na sababu ya jina lake kuchelewa kuingizwa katika mfumo wa usajili wa shirikisho hilo.

Saido anaungana na Tuisila Kisinda ambaye naye amekwama kuingia katika usajili huo baada ya jina lake kutoonekana katika orodha ya wachezaji 39 wa klabu ya Yanga sc ambapo alipaswa kuchukua nafasi ya mshambuliaji Lazarus Kambole ambaye ana majeraha.

banner

Licha ya maneno makali na migongano ya mashabiki wa soka nchini bado mpaka sasa suala hilo la usajili halijafikia muafaka ambapo kamati ya sheria na hadhi za wachezaji inatarajiwa kukaa hivyi leo kutoka majibu ya mwisho kuhusu sajili hizo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited