Home Makala Serikali Yaongeza Kodi Kwenye Mikeka

Serikali Yaongeza Kodi Kwenye Mikeka

by Sports Leo
0 comments

Serikali imeongeza kiwango cha kodi kwa washindi wa michezo ya kubashiri (Betting) kwenye bajeti ya serikali kuu iliyosomwa jana bungeni ili kuongeza mapato kwa serikali.

Waziri wa Fedha Dkt.Mwigulu Nchemba amesema kuwa  Ongezeko la kiwango hicho cha fedha kitakachopatikana, asilimia 70 itaenda katika mfuko wa serikali kupambana na Ukimwi na asilimia 30 kuchangia mfuko wa bima ya afya.

“Kufanya marekebisho kwenye sheria ya michezo ya kubahatisha sura namba 41. Kuongeza kiwango cha kodi kwenye zawadi ya ushindi kutoka asilimia 10 hadi asilimia 15,” amesema Waziri Mwigulu Nchemba bungeni Dodoma leo wakati akisoma bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026.

banner

Tangu serikali iliruhusu michezo ya kubashiri nchini kuanzia mwaka 2015 ambapo imekua ikitunga sheria mbalimbali ili kuratibu michezo sambamba na kuhakikisha kuwa mapato yanapatikana kwa wingi.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited