Home Soka Simba Sc Gari Limewaka

Simba Sc Gari Limewaka

by Sports Leo
0 comments

Sasa Furaha na Shangwe zimerejea kwa mashabiki wa Simba sc baada ya timu hiyo kupata ushindi kwa mara ya pili mfululizo katika mechi za ligi kuu ya Nbc nchini ambapo imeifunga Fountain Gate Fc kwa mabao 4-0 mchezo uliofanyika katika uwanja wa Kmc Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Simba sc chini ya kocha Fadlu Davis haikua na mabadiliko makubwa ambapo ilianza na kipa Camara akisaidiwa na mabeki Shomari Kapombe,Mohammed Hussein,Abdulrazak Hamza sambamba na Che Malone Fondoh huku eneo la kiungo likiwa na Mzamiru Yassin,Deborah Fernández wakisaidiwa na Jean Charles Ahoua,Awesu Awesu na Edwin Balua.

Balua alianza kufungua kalamu ya mabao dakika ya 14 akiunganisha krosi ya Jean Charles Ahoua aliyewazidi maarifa walinzi wa Fountain Gate Fc na kupiga krosi iliyounganishwa kiufundi na Balua.

banner

Dakika ya 44 Shomari Kapombe alimpa pasi safi Steven Mukwala aliyefunga bao la pili kwa Simba sc huku likiwa la kwanza kwake katika ligi kuu ya Nbc.

Jean Charles Ahoua dakika ya 58 alitumia maarifa binafsi kuwahadaa walinzi wa Fountain Gate Fc na kupiga mpira kuitafuta kona ya goli na kumshinda kipa Fikirini Bakari kuucheza mpira huo.

Wakati Fountain Gate Fc wakijipanga kujibu mashambulizi walijikuta wakifungwa bao la nne na Valentino Mashaka dakika ya 81 ya mchezo baada ya kupiga shuti lililomshinda kipa Fikirini Bakari.

Simba sc sasa imejikita kileleni mwa msimamo ikiwa na alama sita huku Jean Charles Ahoua akionyesha mchango mkubwa ambapo mpaka sasa amefunga bao moja huku akitoa asisti tatu katika michezo miwili mpaka sasa.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited