Table of Contents
Yanga Sc Yakubali Kumuuza Mzize
Klabu ya Yanga sc imekubali dau la takribani bilioni mbili za kitanzania ili kumuuza mshambuliaji Clement Mzize kwenda klabu ya Al Sadd inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Qatar.
Mabosi wa Yanga sc baada ya kugomea ofa kadhaa za kumuuza mchezaji huyo ikiwemo ofa mbili kutoka klabu za Al Ittihad ya Libya na Zamaleck Fc ya nchini Misri hatimaye walikubali ofa kutoka katika klabu hiyo maarufu nchini Qatar.
Kipi kinakwamisha Dili hili?
Baada ya kukubali ofa hiyo mabosi wa klabu hiyo walielekeza kuwa sasa klabu hiyo izungumze na Mzize kwa ajili ya kukubaliana maslahi binafsi ili aweze kujiunga na klabu hiyo.
Mpaka sasa ugumu wa dili hilo kukamilika umebaki hapo ambapo mabosi wa Al Sadd wamempa ofa ya mshahara wa shilingi za kitanzania milioni 75 kwa mwezi huku mchezaji huyo akihitaji kiasi cha shilingi milioni 150 za kitanzania kama mshahara wa kila mwezi.
Mpaka sasa mabosi wa klabu hiyo na menejimenti inayomsimamia mchezaji huyo ipo bado katika mazungumzo kuona namna ya kumaliza mazungumzo hayo ili mchezaji huyo asajiliwe na klabu hiyo.
Hatma ya Yanga Sc Baada ya Kumuuza Mzize
Mpaka sasa Mzize bado ni tegemeo katika safu ya ushambuliaji ya klabu ya Yanga sc akiwa na uhakika wa kuanza katika kikosi cha kwanza licha ya uwepo wa Prince Dube ambaye ndie mshambuliaji kiongozi ambapo wote msimu uliopita walifunga mabao 13 kila mmoja.
Jeuri ya Yanga sc kumuuza mshambuliaji huyo inaletwa na usajili wa mshambuliaji Celestine Ecua kutoka nchini Ivory coast pamoja na winga Kouma ambaye naye anaweza kucheza nafasi ya Mzize pamoja na Offen Chikola aliyesajiliwa msimu huu.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Dili hilo linapaswa kukamilika mapema ili Yanga sc ianze kumtoa kwenye kikosi chao kwa kuanza kutengeneza mifumo mingine ya ushambuliaji bila staa huyo ambapo endapo litachelewa basi mabosi wa Yanga sc wanaweza kughairisha mpaka mwakani.
Historia ya Clement Mzize kutoka Iringa Hadi Kuwa Tegemezi Yanga Sc
Mzize aliibuliwa na Yanga sc kipindi cha uongozi wa Dkt.Mshindo Msolwa ambaye alikabidhiwa na wazee wa Iringa ambao waliamini kuwa ana kipaji cha hali ya juu ambapo baada ya kujiunga na Yanga Sc alianzia katika timu ya vijana ya klabu hiyo.
Baada ya muda kocha Mwinyi Zahera alianza kumuamini na kumpa nafasi mara kadhaa lakini kocha Nasredine Nabi aliamua kumuingiza kikosi cha wakubwa moja kwa moja na kuanza kumtumia.
Makocha waliofuata wakiwemo Miguel Gamondi waliona kipaji cha na kuanza kumpa nafasi moja kwa moja katika kikosi cha kwanza na sasa ni moja ya mastaa tegemeo katika ngazi ya klabu na timu ya Taifa ya Tanzania.
Kwa sasa mchezaji huyo yupo katika kambi ya timu ya Taifa ya michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) ambapo amekua kama mshambuliaji kiongozi.
Yanga Sc Yakubali Kumuuza Mzize: Je, Mbadala wake Utatosheleza na kukidhi Viwango alivyoweka
Timu ya Yanga Sc imefanya usajili wa washambuliaji kadhaa hivi karibuni kujiandaa na msimu wa 2025/2026. Usajili wa kimkakati kuwezesha timu hiyo kutwaa makombe yaliyopo mbele yao ikiwemo malengo haswa ni klabu bingwa barani Africa. Kuondoka kwa Mzize ambaye ni tegemezi katika safu ya ushambuliaji kumezua gumzo kwa mashabiki wakihofia kushuka kwa kiwango cha timu yao upande wa mashambulizi. Ukweli ni kwamba licha ya Yanga Sc kukubali kumuuza Mzize, imejipanga vyema na kupata mbadala sahihi wa safu ya ushambuliaji Yanga Sc. Usajili mpya unalenga kuboresha na kuziba pengo la Mzize kama atafanikiwa kuondoka klabuni hapo.
Sajili mpya zitatosheleza kiu ya magoli na kuziba pengo la Mzize kwa kiwango kile kile ama cha juu zaidi. Takwimu zinawabeba wachezaji hawa wapya Andy Boyeli, Celestin Ecua na Mohamed Doumbia ambaye wanatabiri kuwa mrithi sahihi wa kuziba nafasi ya Azizi Ki aliyetimkia Wydad. Pia washambuliaji hawa wapya wanaweza kuziba pengo la Clement Mzize kama atauzwa.