Home Soka Zahera Amkataa Ajibu Yanga

Zahera Amkataa Ajibu Yanga

by Sports Leo
0 comments

Kocha mkongomani wa Yanga Mwinyi Zahera amewashangaa viongozi wa timu hiyo kuanza mazungumzo na Mshambuliaji Ibrahim Ajib ili kuongeza mkataba wa kuitumikia klabu hiyo ya Jangwani baada ule wa awali kufikia kikomo msimu huu.

Kocha huyo mwenye misimamo mikali ambaye mbali ya kuifundisha Yanga pia ni kocha msaidizi wa Timu ya Taifa ya Kongo amesema kuwa mshambualiaji huyo hayupo katika ripoti ya wachezaji anaowahitaji kwa msimu ujao kwani alijua anajiunga na Tp Mazembe hivyo hamhitaji kikosini hapo na hata kama hajajiunga na wakongomani hao.

Zahera ambaye amekua akikubali kipaji cha Ajib na kumshangaa mchezaji huyo kuendelea kuwepo Tanzania ni kocha muumini mkubwa wa nidhamu kwa wachezaji wake huku akiifanya Yanga kuwa timu kali licha ya kuwa na kikosi cha kawaida na hali ngumu ya kiuchumi.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited