Mwacheni Gamondi Aende na Machaguo Yake Afcon

Jikubali Pokea ⚽️.timuyawananchidaimambelenyumamwikoByutiByutiyangasc tanzaniaV totalen

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Miguel Gamondi, ameendelea kusimamia falsafa yake ya kuchagua wachezaji kwa kuangalia uimara, uzoefu na utulivu wa kiuchezaji badala ya kelele za mitandaoni au presha za mashabiki.

Katika kuitengeneza timu yake kuelekea michezo ijayo ya michuano ya mataifa ya Afrika 2025, Gamondi ameenda na majina matatu kwenye upande wa kulia wa ulinzi: Shomari Kapombe, Lusajo Mwaikenda na Haji Mnoga. Ingawa mijadala imekuwa mikubwa kuhusu kutomuita Israel Patrick Mwenda, uchambuzi wa kina unaonesha kuwa bado kuna sababu nzito ambazo zimefanya kocha achague wachezaji hawa watatu.

Kwanza, Shomari Kapombe, licha ya kuelekea mwisho wa career yake, bado anabaki kuwa mmoja wa mabeki wa kulia wenye uelewa mkubwa wa mchezo ndani ya eneo la ulinzi. Ni mchezaji ambaye anajua kusoma mpira, ana uzoefu wa mechi kubwa, na bado ana uwezo wa kupandisha timu kwa utulivu na maamuzi sahihi. Kutokana na uzoefu wake ndani ya Taifa Stars na klabu ya Simba, Kapombe anabaki kuwa chaguo linaloaminika zaidi, hasa kwenye mechi ambazo zinahitaji utulivu na maamuzi ya busara. Hata ukimlinganisha na Mwenda, ni wazi kuwa kiufundi na kimtazamo wa mechi kubwa, Kapombe bado yuko juu licha ya umri na kupungua kwa kasi.

587624140 18522414889071034 5155789479155709204 n 1

Pili, Lusajo Mwaikenda ambaye amekuwa akicheza kwenye timu ambayo haina mashabiki wengi kama Simba sc na Yanga sc, anaendelea kupuuzwa sana kwenye mijadala ya mashabiki. Lakini kiuchezaji, Mwaikenda ana nguvu, kasi na maamuzi ya uhakika anapokuwa kwenye mipira ya kujilinda. Ana uwezo mzuri wa kupandisha mashambulizi na ni mchezaji anayefuata maelekezo ya kocha kwa umakini mkubwa. Uwezo wake wa kukaba mtu mmoja mmoja (one-on-one defending) unatajwa kuwa bora zaidi kuliko wa Mwenda kwa sasa. Hii inafanya uwepo wake kwenye kikosi kuwa na uzito, hasa kwa kocha anayehitaji uwajibikaji wa hali ya juu kwenye nafasi za ulinzi.

MUNGU NI MWEMA WAKATI WOTE🙏 📸 @cadorito

Tatu, Haji Mnoga ni mchezaji kijana lakini mwenye kupanda chati kwa kasi. Kwenye kikosi cha Taifa Stars amekuwa akionesha uthubutu, nguvu na uwezo mkubwa wa kupambana kwenye mechi za kiwango cha juu. Mnoga ana faida ya umri, stamina na uwezo wa kurudi kwenye eneo lake kwa wakati (recovery speed), kitu ambacho kocha Gamondi anakithamini sana. Kwa tathmini ya kiufundi, hata kama Mwenda yuko kwenye form nzuri, bado Mnoga anaonekana kumzidi kwenye maeneo kadhaa ya kiuchezaji yanayohitajika katika soka la kimataifa.

🦁🔴

Israel Mwenda amekuwa akifanya kazi nzuri ndani ya Yanga SC, akicheza kama chaguo la kwanza kwenye mechi nyingi za ligi. Ameonesha kukua kiochezaji na kupata ujasiri mkubwa akishambulia upande wake. Hata hivyo, ndani ya mfumo wa timu ya taifa, bado kuna hisia kwamba Mwenda ana kazi ya kufanya ili kufikia kiwango cha kuogopwa (threat level) anapovuka nusu ya uwanja. Kuna nyakati ambapo maamuzi yake ya mwisho hayajawa na uzito ule ule wanaokuja naye kwenye nafasi hiyo.

Hii haimaanishi Mwenda si mchezaji mzuri la hasha. Ni mchezaji mwenye kipaji halisi, maono mazuri na mustakabali mkubwa. Ila kwa sasa, kiuchezaji, bado watu watatu waliochaguliwa wanamzidi kwenye eneo moja au mawili muhimu ambayo kocha Gamondi anayapa kipaumbele. Ndiyo maana hoja kwamba Mwenda hapaswi kukosa timu ya taifa bado inakuwa na mjadala mpana, lakini kiufundi, maamuzi ya kocha yana mantiki.

Kwa kifupi, kelele za mashabiki ni sehemu ya mpira, lakini mwisho wa siku kocha huchagua anachokiona kinamfaa ndani ya mfumo wake. Kwenye upande wa kulia, Mwenda bado hajawagusa hawa watatu kiuwezo wa moja kwa moja. Hii ni changamoto kwake kuendelea kupambana, kuboresha sehemu zake dhaifu na kuhakikisha anakuwa chaguo lisilopingika ndani ya klabu na pia Taifa Stars.

Leave a Reply

Enable Notifications OK No thanks