Mwenda Asalia Yanga Sc

Beki Israel Mwenda ameamua kusalia katika klabu ya Yanga Sc baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu hadi mwaka 2028 ndani ya klabu hiyo yenye makazi yake Jangwani jijini Dar es Salaam.
Awali beki huyo alikuwa na mpango wa kurejea Singida Black Stars endapo Ofa na mahitaji yake yyasingekubaliwa na mabosi wa klabu hiyo lakini sasa kila kitu kipo sawa.
Mwenda aliondoka Simba Sc na kujiunga na Singida Black Stars ambayo nayo iliamua kumtoa kwa mkopo wa miezi sita kwenda Yanga sc ambayo sasa imemalizana na Singida Black Stars kwa kumnunua moja kwa moja.
Mwenda ana uhakika wa nafasi kwa upande wa beki wa kulia kikosini humo akifanikiwa kufunga mara kadhaa akimuweka benchi Kibwana Shomari ambaye alikua anaanza mara kwa mara huku kuumia kwa Yao Kouassi kukitoa nafasi kwa vijana hao wa kitanzania.
Bahati iliyoje kwa beki huyo ambapo msimu huu amefanikiwa kutwaa mataji yote matatu ya ndani na moja la Muungano Cup Visiwani Zanzibar akiwa na Yanga sc.

