Home Soka Balinya,Sadney Kuwaua Rollers

Balinya,Sadney Kuwaua Rollers

by Sports Leo
0 comments

Imefahamika kwamba mganda Juma Balinya na Sadney Urikhob ndi wataongoza safu ya ushambuliaji ya Yanga kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi Township Rollers ya Botswana uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Kupitia michezo mbalimbali ya kirafiki ambayo timu hiyo imecheza ukiwemo wa siku ya mwananchi dhidi ya Kariobang Sharks ambapo kocha mkuu wa timu hiyo alikaa benchi kwa mara ya kwanza aliwaanzisha mastraika hao wawili huku wakisaidiwa na Balama Mapinduzi na Patrick Sibomana kama mawinga wapembeni.

banner

Kwa upande wa kiungo bila shaka mkongo Papy Tshitshimbi ataongoza safu hiyo huku ikitemewa atasaidiwa na kati ya Feisal Salum au Mohamed Banka japo Banka ana nafasi kubwa ya kuanza kutokana na kutengeneza kombinesheni nzuri na mkongo huyo.

Lamine Moro na Ally Sonso wana uhakika wa kuanza katika beki ya kati kutokana na mkongwe Kelvin Yondani kutokuwepo kikosini  huku ikiripotiwa matatizo ya kifamilia yamesababisha wakatai Andrew Vicent na Juma Abdul wakisubiri kukamilishiwa madai yao ndipo wajiunge na timu.

Paul Godfrey,Mohamed Mwalami na Farouk Shikalo nafasi zao hazina mpinzani mpaka sasa na wanatarajiwa kuanza katika kikosi hicho kulingana na uwezo waliouonyesha katika mechi za kirafiki hasa dhidi ya Mlandege ikilinganishwa na wengine waliopo kikosini hapo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited